Movies
Auditory Test Instructions
Karibu kwenye Auditory T.O.V.A. Jaribio
Shika kitufe kwenye mkono wako wa kuandikia huku kidole gumba kikiwa kimetulia kiasi juu ya kitufe, hivi.
Unapobonyeza kitufe, achilia pindi tu unaposikia bofya; si lazima ukishikilie chini.
Bonyeza kitufe ukiwa tayari kuendelea.
Jaribio hili hupima uwezo wako wa kumakinika.
Sauti mbili tofauti zitachezwa kwenye spika.
Sauti moja ni ya juu, hivi:
...na nyingine ni sauti ya chini, hivi:
Sauti zitachezwa kila baada ya sekunde chache, hivi:
Bonyeza kitufe haraka uwezavyo kila wakati unaposikia sauti ya juu...
...na usibonyeze kitufe unaposikia sauti ya chini.
Kwa mara nyingine, bonyeza kitufe pekee unaposikia sauti ya juu.
Usibashiri sauti itakayocheza; hakikisha kuwa umeisikia kabla ya kubonyeza kitufe.
Jaribu kusawazisha sauti na usahihi: bonyeza kitufe haraka uwezavyo, lakini pia hakikisha kuwa hukosei.
Ukikosea, usijali: yeyote anaweza kukosea kwenye jaribio hili.
Hebu tuhakiki:
✓ Bonyeza kitufe haraka uwezavyo, lakini tu ukisikia sauti ya juu.
✓ Unapobonyeza kitufe, kibonyeze mara moja pekee na usikishikilie chini. “Bofya” kitufe tu.
✓ Mwisho, usiharakishe sana wala kujaribu kubashiri; chukua muda wa kutosha kuamua ni sauti gani.
Auditory Pre-Practice Test Instructions
Unakaribia kufanya jaribio fupi la utendaji.
Baada ya kuhesabu, sauti itaanza kucheza.
Kumbuka, harakisha na uwe sahihi uwezavyo.
Bonyeza kitufe ukiwa tayari kuanza.
Auditory Pre-Test Instructions
Unakaribia kufanya jaribio la T.O.V.A, ambalo litachukua dakika 20.
Huenda ukatambua kuwa unachoka kidogo. Hata hivyo, jaribu na ufanye vyema uwezavyo.
Kumbuka kubonyeza kitufe haraka uwezavyo, lakini wakati tu ambapo unasikia sauti ya juu.
Bonyeza kitufe ukiwa tayari kuanza.