TOVA Test Instructions (Swahili)

Movies

Visual Test Instructions

Karibu kwenye Visual T.O.V.A. Jaribio


Shika kitufe kwenye mkono wako wa kuandikia huku kidole gumba kikiwa kimetulia kiasi juu ya kitufe, hivi.

Unapobonyeza kitufe, achilia pindi tu unaposikia bofya; si lazima ukishikilie chini.

Bonyeza kitufe ukiwa tayari kuendelea.


Jaribio hili hupima uwezo wako wa kumakinika.


Miraba miwili tofauti itaonekana kwenye skrini.

Mraba moja una mraba mdogo mweusi karibu na sehemu ya juu...

...na nyingine ina mraba mdogo karibu na sehemu ya chini.

Miraba itaonekana kwenye skrini, hivi:


Bonyeza kitufe haraka uwezavyo kila wakati unapoona mraba wenye mraba mdogo karibu na sehemu ya juu...

...na usibonyeze kitufe wakati mraba mdogo uko karibu na sehemu ya chini.

Kwa mara nyingine, bonyeza kitufe pekee unapoona mraba mdogo karibu na sehemu ya juu.


Usibashiri mraba utakaoonekana; hakikisha kuwa umeuona kabla ya kubonyeza kitufe.

Jaribu kusawazisha sauti na usahihi: bonyeza kitufe haraka uwezavyo, lakini pia hakikisha kuwa hukosei.

Ukikosea, usijali: yeyote anaweza kukosea kwenye jaribio hili.


Hebu tuhakiki:

Bonyeza kitufe haraka uwezavyo, lakini tu ukiona mraba mdogo karibu na sehemu ya juu.

Unapobonyeza kitufe, kibonyeze mara moja pekee na usikishikilie chini. “Bofya” kitufe tu.

Mwisho, usiharakishe sana wala kujaribu kubashiri; chukua muda wa kutosha kuona ni mraba gani.


Visual Pre-Practice Test Instructions

Unakaribia kufanya jaribio fupi la utendaji.

Baada ya kuhesabu, miraba itaanza kuonekana.

Kumbuka, harakisha na uwe sahihi uwezavyo.


Bonyeza kitufe ukiwa tayari kuanza.


Visual Pre-Test Instructions

Unakaribia kufanya jaribio la T.O.V.A, ambalo litachukua dakika 20.

Huenda ukatambua kuwa macho yako yanachoka kidogo. Hata hivyo, jaribu na ufanye vyema uwezavyo.

Kumbuka kubonyeza kitufe haraka uwezavyo, lakini wakati tu ambapo mraba mdogo uko karibu na juu.


Bonyeza kitufe ukiwa tayari kuanza.